MASHINDANO VIJANA KWA USALAMA KWA VIJANA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUPITIA VIDEO BLOG


 

MASHINDANO VIJANA KWA USALAMA KWA VIJANA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUPITIA VIDEO BLOG

Wakati Helen Clark wa  UNDP aliposema maendeleo  hayawezi kupatikana kama asilimia  hamsini (50%) ya idadi ya watu  kwa kuwa wametengwa kutokana na fursa zinayotolewa,  alikuwa akimaanisha kuwawezesha wanawake kuwa na uwezo  sawa  wa kushiriki katika maamuzi ndani  ya jamii.

Katika Afrika ya leo, kuna watu ambao  bado hawajasikizwa wakiwemo vijana wa Afrika. Katika maeneo mengi ya Afrika zaidi ya  asilimia hamsini (50%) ya wakazi ni watu wenye umri wa  chini ya  miaka ishirini na tano (25), na kwa bahati mbaya,  maoni yao, uzoefu na mapendekezo ya kuboresha usalama ndani ya jamii mara kwa mara upita bila kusikilizwa.

Lengo letu ni kubadilsha jambo hili kupitia mashindano ya vijana kwa usalama wa jumuiya ya afrika mashariki video blog (EAY4S) Dhana nzima ya ushindani huu wa EAY4S ni kujenga jukwaa la kuruhusu uhuru wa kujieleza kupitia  maoni, uzoefu na mapendekezo kwa watu wenye umri usiozidi miaka ishirini na mitano (25) na kwa jamii iliyo salama. Hii ni kwa  vijana waliopo  ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  ikiwemo-Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda.  wanaweza kushiriki katika mashindano haya kwa kurekodi na kuwasilisha video yako kwa kujibu moja kati ya mada nne tajwa za kiusalama kama ifuatavyo.

1) Uhandisi – Ni mabadiliko gani ambayo unaweza  kuyapendekeza ili kuboresha usalama wa miundombinu ya barabara, majengo, na / au mashine katika jamii yako? Ni  maboresho gani fanisi yanahitajika katika maeneo/mazingira unayoishi?

2) Elimu – Ni mikakati gani wa kielimu unaoweza  kukuza na kuendeleza usalama ndani ya jamii yako? Ni njia zipi sahihi na zenye ufanisi zaidi zitumike katika sehemu unayoishi?  Ni nani watakuwa walengwa?

3) Msukumo – Ni mkakati gani unaweza kutumika kuleta msukumo wa kuimarisha usalama katika jamii. Walegwa watakuwa nani? Ni eneo gani utakuwa unaweza kulimudu vizuri

4) Uchumi – Ni mbinu gani za kiuchumi zinazoweza kutumika kuhimiza na kuboresha usalama kwa jamii yako?

Video maoni ya msingi kuhusu mada nne tajwa hapo juu yanaweza kutayarishwa kwa  kutumia kamera ya simu, kamera za mtandao au kifaa kingine  chochote cha kurekodi video.

Kisha video inaweza kuwekwa kakika mtandao wa YouTube na kuunganishwa nasi pia kupitia earscc2014@peercorpstrust.org

Ni  lazima itumwe kwa lugha ya Kiingereza ili majaji wetu wa kimataifa waweze kuzichambua.

Video zote lazima ziwe na muda wa dakika 3.

Washindi watatuzwa kama ifuatavyo, nafasi ya kwanza atapata Dola za kimarekani $ 300 Mshindi wa pili atapata dola za kimarekani $ 200 na wa tatu dola za kimarekani $ 100

Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha video hizo ni Tarehe 01/10/2014

Washindi watatangazwa kupitia tovuti ya PEERVoice Blog ambayo ni  www.peercorpsglobal.org tarehe  10/10/2014.

Leave a Reply